Leo ni Siku ya Pasaka
Leo ni Siku ya Pasaka Lyrics
- Leo ni siku ya Pasaka, tumshangilie Bwana wetu -
Leo ni siku ya Pasaka, tumshangilie Bwana wetu
Mwanakondoo aliyekufa atawala mzima leo
Aleluya Bwana Yesu leo ameshinda kifo *2
Aleluya Bwana Yesu leo amshinda kifo *2
Yesu tumaini (letu) kafufuka mfalme (wetu)
Sote na tuimbe, (hosanna) tukimsifu Mfalme (wetu)
Aleluya Bwana Yesu leo ameshinda kifo
- Kristu mshindaji wetu atupatanisha na Baba
Katika wafu ametoka tumshangilie Bwana wetu
- Maria Magdalena tuambie ni nini ulichoona leo
Niliona kaburi tupu sanda na nguo zimebaki
nikawaona malaika wakitangaza ufufuko
Niliona kaburi tupu sanda na nguo zimebaki
nikawaona malaika wakitangaza ufufuko
Sasa nasi tuombe atusaidie tushinde pia
Kristu uliyefufuka utuhurumie na sisi
Kristu uliyefufuka utuhurumie na sisi