Asubuhi na Mapema
| Asubuhi na Mapema |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 6,228 |
Asubuhi na Mapema Lyrics
Asubuhi na mapema, siku ya kwanza ya juma
Wanawake walikwenda kaburini
Wakiwa na mafuta na manemane
Ili wampake Bwana ilivyo desturi *2
Pale kaburini walishikwa na mshangao
Kaburi li wazi hafungwi
Mwokozi ametoka mzima
Kafufuka alivyosema
- Kufika pale kaburini, waliona li wazi
Wakabaki wakilia, ati Bwana wamemchukua
- Jiwe lilikuwa kando, ndani vimo vitambaa
Alivyofunikwa Bwana, kweli Bwana amefufuka
- Tufurahi watu wote Bwana wetu kafufuka
Katuondolea dhambi kweli tuimbe aleluya