Kuteswa Kwake Bwana
| Kuteswa Kwake Bwana | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 13,167 | 
Kuteswa Kwake Bwana Lyrics
- Kuteswa kwake Bwana kulinipa wokovu
 Siachi kumuimbia pote niendapo *2
- Aliyeniokoa ni Yesu aliyevumilia mateso
 aliyemwaga damu mtini ndiye Bwana wangu *2
- Na kwa kunipenda mimi, aliuawa akafa
 Ni pendo la ajabu kunifilia *2
- Rohoni nimeoshwa na damu ya thamani
 Makosa yameoshwa naye Mwokozi *2
 
  
         
                            