Uniokoe Uniokoe
Uniokoe Uniokoe |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 3,336 |
Uniokoe Uniokoe Lyrics
Unioke uniokoe na watu hao wabaya
Na unikinge unikinge na wakatili
Wenye mawazo mabaya *2
- Daima hao huzusha ugomvi
Na ndimi zao hatari kama nyoka
Midomo yao maneno hatari
Ni kama sumu hatari ya joka
Mwenyezi Mungu naomba unilinde
Kwa kucha zao wabaya na katili
- Wenye kiburi hutega
Mipango yao waone uanguke
Wametandaza kamba kama wavu
Njiani wamezificha mitego
Mipango yao yote wanikamate
Sauti ya ombi langu sikiliza
- Mkombozi mkuu wangu umenikinga
Salama hata wakati wa vita
Waovu usiwape wanayotataka
Mipango yao mibaya huivunje
Wameinua kucha wamenizingira
Uovu wao wenyewe uwapate