Mwokozi Wangu Rabi
| Mwokozi Wangu Rabi | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 3,499 | 
Mwokozi Wangu Rabi Lyrics
- Mwokozi wangu Rabi
 Hukukosa kitu
 hukuitenda dhambi
 Wapigwa bure tu
 Mwenye dhambi ni mie
 Mie mwenye ovu
 Toba nihurumie
 Nisikose wokovu
- Kwanza sijazaliwa
 Ulinikumbuka
 Mtini kachomewa
 Kwa yangu sadaka
 Na mie nisiwaze
 Nimekuwa mgumu
 Rabi hunigeuza
 Ukome wazimu
- Leo nakuungama
 Ndiwe Mungu wangu
 Mwenye wingi wa neema
 Mkazi wa uwingu
 Sasa nimekupenda
 Muinue mtumwao
 Kwa mambo kuyatenda
 Mpe nguvu na moyo
 
  
         
                            