Mwokozi Wangu Rabi

Mwokozi Wangu Rabi
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Mwokozi Wangu Rabi Lyrics

 1. Mwokozi wangu Rabi
  Hukukosa kitu
  hukuitenda dhambi
  Wapigwa bure tu
  Mwenye dhambi ni mie
  Mie mwenye ovu
  Toba nihurumie
  Nisikose wokovu
 2. Kwanza sijazaliwa
  Ulinikumbuka
  Mtini kachomewa
  Kwa yangu sadaka
  Na mie nisiwaze
  Nimekuwa mgumu
  Rabi hunigeuza
  Ukome wazimu
 3. Leo nakuungama
  Ndiwe Mungu wangu
  Mwenye wingi wa neema
  Mkazi wa uwingu
  Sasa nimekupenda
  Muinue mtumwao
  Kwa mambo kuyatenda
  Mpe nguvu na moyo