Ninakulilia
| Ninakulilia | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 4,820 | 
Ninakulilia Lyrics
- Ninakulilia Bwana Mungu, nipe neema zako
 ili shetani asinishinde, niwe wako milele *2
- Uwe ndani yangu siku zote, Baba usiniache
 Niwe ndani yako siku zote, niwe wako milele
- Haki yako na idumu duniani siku zote
 Uangaze roho yangu nikutii daima
 Ee Baba unilinde
- Ee Baba utazame, dunia yageuka
 Ndugu wauana, magonjwa yamezidi
- Upendo na haupo, kati ya majirani
 Kwa kuwa haya yote, ni mwisho wa dunia
- Ee ndugu tukumbuke (kwamba) raha za duniani (ovyo)
 Kuna faida gani (kweli) kufuata ulimwengu
 Na mwisho tusiishi na Baba Mungu ? *2
 
  
         
                            