Hosanna Mwana wa Daudi
Hosanna Mwana wa Daudi | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Jumapili ya Matawi (Palm Sunday) |
Composer | (traditional) |
Views | 8,763 |
Hosanna Mwana wa Daudi Lyrics
Hosanna Mwana wa Daudi, ndiye mbarikiwa
Yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli
Hosanna juu Mbinguni
Enyi watu wote pigeni makofi
Mshangilieni Mungu kwa shangwe kubwa- Kwa sababu Bwana aliye juu ni mwenye kutisha
Ndiye mfalme mkuu wa dunia yote - Atawatisha watu wa dunia chini yetu
Na mataifa chini ya miguu yetu - Atatuchagulia urithi wetu
fahari ya Yakobo ambaye alimpenda - Mwimbieni Mungu imbeni,
Mwimbieni mfalme wetu mwimbieni - Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote
Imbeni kwa akili - Mungu awamiliki mataifa
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu - wakuu wa dunia wamekusanyika
Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu - Maana ngao za dunia zina Mungu
Ametukuka sana