Kweli Ilimpasa Kristu

Kweli Ilimpasa Kristu
ChoirTBA
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)

Kweli Ilimpasa Kristu Lyrics

{Kweli ilimpasa Kristu ateswe
Na kufufuka katika wafu aleluya } *2

 1. Furahini mkishiriki mateso ya Kristu
  Mtafurahi zaidi atakapofika tena
 2. Ikiwa tulikufa pamoja na Kristu
  Tutaishi pia pamoja naye
 3. Tukiendelea kuvumilia
  Tutatawala pamoja naye
 4. Tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana
  Tukifa tunakufa kwa ajili ya Bwana
 5. Kristu alikufa akafufuka
  Apate kuwa Bwana wa walio hai na wafu
 6. Muwe waamninifu hata mpaka kufa
  Nami nitawapeni taji la uhai