Natamani Paradiso
Natamani Paradiso |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Views | 5,522 |
Natamani Paradiso Lyrics
Natamani kwenda Mbinguni kuiona paradiso (kwa kweli) *2
Mji wake Mungu aloutengeneza makao ya burudani
yenye raha na kucheza
Nitakaza mwendo sana nifike Mbinguni *2
- Bwana Yesu Kristu alituahidi
makao ya Mbinguni, yenye starehe,
Sayuni ya Mbinguni imepambwapamba
kwa dhahabu ya almasi ninatamani (mimi)
- Mimi natamani kuja mbele zako
pahali patakatifu penye sifa tele
Kwenye kiti cha enzi ninakizunguka
nikiwa nimepewa taji la ushindi (mimi)
- Nuru ya Mbinguni si mwezi wala jua
bali ni Yesu Kristu yule Mwanakondoo
Nitamwona masihi mwanga wa Mbinguni,
yeye macho kwa macho alityenifia (mimi)
- Ewe Mungu mwema mwingi wa rehema
nilinde duniani nishinde majaribu
Malaika mlinzi niongoze vyema
nifike paradizo niishi milele (mimi)