Natamani Paradiso

Natamani Paradiso
Performed by-
CategoryTafakari
Views5,272

Natamani Paradiso Lyrics

  1. Natamani kwenda Mbinguni kuiona paradiso (kwa kweli) *2
    Mji wake Mungu aloutengeneza makao ya burudani
    yenye raha na kucheza
    Nitakaza mwendo sana nifike Mbinguni *2

  2. Bwana Yesu Kristu alituahidi
    makao ya Mbinguni, yenye starehe,
    Sayuni ya Mbinguni imepambwapamba
    kwa dhahabu ya almasi ninatamani (mimi)
  3. Mimi natamani kuja mbele zako
    pahali patakatifu penye sifa tele
    Kwenye kiti cha enzi ninakizunguka
    nikiwa nimepewa taji la ushindi (mimi)
  4. Nuru ya Mbinguni si mwezi wala jua
    bali ni Yesu Kristu yule Mwanakondoo
    Nitamwona masihi mwanga wa Mbinguni,
    yeye macho kwa macho alityenifia (mimi)
  5. Ewe Mungu mwema mwingi wa rehema
    nilinde duniani nishinde majaribu
    Malaika mlinzi niongoze vyema
    nifike paradizo niishi milele (mimi)