Ukarimu wa Bwana Yesu
Ukarimu wa Bwana Yesu |
---|
Alt Title | Nani kama Bwana Yesu |
Performed by | - |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | Stanslaus Mujwahuki |
Views | 13,833 |
Ukarimu wa Bwana Yesu Lyrics
- Nani kati ya watala wote, wafalme wa dunia hii
Aliyewahi kuandaa karamu, akaalika watu wote
{ Ni nani kama Bwana Yesu, mfalme wa mbingu na nchi
Anayetualika sote kwenye karamu aliyoiandaa,
bali tuwe na moyo safi } *2
- Sote tunaalikwa kushiriki, kwenye karamu yake Bwana,
Tukiwa tajiri au masikini, bali tuwe na moyo safi.
- Ishara ya mapendo makubwa kwetu, kutoka kwake Bwana Yesu
Kutoa mwili kutoa damu yake, kuzishibisha Roho zetu
- Ni fundisho kutoka kwake Bwana, tuuonyeshe ukarimu
kwa ndugu rafiki au majirani, daima maishani mwetu