Ni Nani Hawa

Ni Nani Hawa
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerD. Kalolela
SourceTanzania

Ni Nani Hawa Lyrics

Ni nani hawa watembeao kwa furaha
Wakiijongea altare
Ni wateule wake Bwana walioalikwa kwa karamu

  1. Yakupasa ujiulize ndugu una kikwazo gani
    kinachokufanya uiogope meza ya Bwana
  2. Hebu watazame wenzako wanavyokwenda kwa furaha
    Wakiijongea meza ya Bwana kwa karamu
  3. Bwana Yesu ameutoa mwili wake kuwa chakula
    Na damu yake kaitoa kwetu kama kinywaji