Wastahili Kusifiwa

Wastahili Kusifiwa
Performed by-
AlbumKanisa Linalosafiri
CategoryGeneral
ComposerG. A. Miyombo
Views4,504

Wastahili Kusifiwa Lyrics

  1. {Wastahili, wastahili kusifiwa ee Bwana
    kusifiwa na kutukuzwa na viumbe vyako }*2

    Mbingu na dunia zimejaa sifa zako, sifa zako ee Bwana *2
    {Pokea masifu ya viumbe vyako - uhimidiwe milele aleluya
    Bwana wa mabwana - uhimidiwe - uhimidiwe milele aleluya }*2

  2. Malaika mbinguni wanakuhimidi wewe wakusifu milele, ee Bwana
  3. Milima na mabonde, miti yote ya porini vyakusifu milele, ee Bwana
  4. Wanyama wa porini na wanyama wafugwao wakusifu milele, ee Bwana
  5. Samaki baharini nao ndege wa angani wakusifu milele, ee Bwana