Yesu Ateswa Msalabani
| Yesu Ateswa Msalabani |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Composer | Fr. G. F. Kayeta |
| Views | 4,124 |
Yesu Ateswa Msalabani Lyrics
- Tunapoona Bwana Yesu kuteswa msalabani
Tunasikitika kweli
Kwani tumekusulubu ee Bwana utuhurumie
- Dhambi zetu nyingi sana asili ya mateso
Watupenda mpaka mwisho
Umekufa tuokoke ee Bwana utuhurumie
- Tunapona msalabani sawa na mwizi mbaya
Ulitaka kutukanya
Tuyaache majivuno, ee Bwana utuhurumie
- Tunapoona msalabani miiba yachoma kichwa
Unalipa kwa matesa
Fungua na tamaa zetu ee Bwana utuhurumie
- Msalabani, umefungwa na mikono ya damu
Mkono wako wenye heri
Utujaze na baraka, ee Bwana utuhurumie
- Mwili wote wafunikwa, na damu ivujayo
Damu yako isafishe
Uovu wote wa rohoni, ee Bwana utuhurumie
- Moyo wako umetonwa, mlango sasa wazi
Tutakase tuingie,
Tukae moyoni mwako, ee Bwana utuhurumie