Uzuio wa Umeme
| Uzuio wa Umeme |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Views | 2,761 |
Uzuio wa Umeme Lyrics
Uzuio wa umeme, mlinzi wa Kimasai
Mbwa mkali tunguri na silaha za kisasa
hakika, hazifai kitu, kweli hazifai kitu
Bwana amtumapo mjumbe kuchukua roho yako
- Wako wapi, wako wapi waliowahi kutikisa dunia?
Wako wapi walioita miungu na dunia?
Na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kujikinga
Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua?
- Wako wapi, wako wapi waliowahi kuishi angani?
Wako walio ishi kwenye madaha?
Je hakuna hata mmoja wao aliyeweza kujificha
Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua