Uzuio wa Umeme Lyrics

UZUIO WA UMEME

Uzuio wa umeme, mlinzi wa Kimasai
Mbwa mkali tunguri na silaha za kisasa
hakika, hazifai kitu, kweli hazifai kitu
Bwana amtumapo mjumbe kuchukua roho yako

 1. Wako wapi, wako wapi waliowahi kutikisa dunia?
  Wako wapi walioita miungu na dunia?
  Na hakuna hata mmoja wao aliyewahi kujikinga
  Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua?
 2. Wako wapi, wako wapi waliowahi kuishi angani?
  Wako walio ishi kwenye madaha?
  Je hakuna hata mmoja wao aliyeweza kujificha
  Bwana alipomtuma mjumbe kumchukua
Uzuio wa Umeme
CATEGORYTafakari
 • Comments