Twakukimbilia Maria Mama

Twakukimbilia Maria Mama
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumNakupenda Maria
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu
SourceTanzania

Twakukimbilia Maria Mama Lyrics

 1. Twakukimbilia Maria, mama Bikira mwenye huruma
  Tutie nguvu ya safari, tufike kwa mwanao Yesu Kristu

  Angaza njia Mama Maria,
  Tufike makao ya uzima
  Giza limeyafunika macho
  Mama Maria Mama Maria, twapotea,
  Tunahitaji msaada wako
  Mama Maria Mama Maria, tuone njia

 2. Safari ngumu Maria, shetani mwovu atusumbua
  Hatua ni nzito Maria, miguu yetu imelegea
 3. Utupe nguvu Maria, ili tusije vunjika moyo
  Tuwe shupavu na imara, katika safari hii ya roho
 4. Utuombee kwa mwanao, tupate nguvu kumshinda shetani
  Tujikane tujute dhambi, tuweze kufika kwake mbinguni