Ombi Moja

Ombi Moja
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
CategoryBikira Maria
ComposerB. Byabato
SourceTanzania

Ombi Moja Lyrics

Ombi moja twalileta kwako ee Maria (mama yetu)
Tujalie kufika mbinguni uliko mama
Tufurahi na watakatifu milele yote

 1. Safari ni ndefu na magumu ni mengi
  Mama tupe neema ya kufaulu
 2. Dhambi zetu nyingi zinatusonga sana
  Tujalie neema ya kuokoka
 3. Hila za shetani na majaribu yake
  Zatukinga njia kufika kwako
 4. Pia twaombea na wasiokujua
  Uwasaidie kufika kwako