Niongoze Vyema Maria

Niongoze Vyema Maria
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumAsante Mama wa Yesu
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu
SourceTanzania

Niongoze Vyema Maria Lyrics

 1. Nahangaika hapa duniani, maisha yangu hayana furaha
  Najua wazi hapa si nyumbani, bali njia ya kupita

  Niongoze vyema Maria, maria Mwema
  Bondeni huku niliko nifike kwa usalama
  Mbinguni kwa Yesu mwanao

 2. Vita na shari vyote vyanisonga, mashaka mengi yaniingia
  Mwili a roho havina kinga hatari imezidia
 3. Mama Maria ndiwe jibu langu hapa safarini unisaidie
  Unipombee kwa mwanao Yesu anikinge anilinde
 4. Kwa kuwa Yesu ni Mwokozi wangu nakusihi Mama
  Nakusihi sana uzifikishe kwake shida zangu anionee huruma
 5. Kumbuka Mama, Yesu alisema, Mama yangu Mwema
  Tazama mwanao, nawe Yohana huyu ndiye mama yako