Ewe Mama Maria Umebarikiwa
| Ewe Mama Maria Umebarikiwa |
|---|
| Performed by | - |
| Category | TBA |
| Views | 3,130 |
Ewe Mama Maria Umebarikiwa Lyrics
{Ewe Mama Maria umebarikiwa,
Mama mwenye huruma, utuombee} *2
- Umebarikiwa Mama wa Mungu
Mama wa Mwokozi Mama wa Yesu
Utuombee Mama mwenye huruma
- Uwinguni juu unapoketi
Na mwanao Yesu anatawala
Utuombee Mama utuongoze
- Adui shetani ametubana
Utukinge na hila zake
Utuombee mama mwenye huruma
- Na siku ya mwisho usiwe mbali
Kufa peke yetu sikubali
Mama mwenye huruma utuombee
- Mama wetu bora tunakusifu
Na huko Mbinguni wakuheshimu
Utuunganishe ee Mama mwema