Twausifu Moyo wako Maria

Twausifu Moyo wako Maria
Performed byKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
AlbumUwe Nasi Mama Maria
CategoryBikira Maria
Views5,214

Twausifu Moyo wako Maria Lyrics

  1. Twausifu, moyo wako Mama Maria, (moyo mwema )
    Twauheshimu, moyo wako mama Maria (moyo safi)
    Moyo wako Maria usio na doa
    Moyo wako Maria usio na doa

  2. Moyo wako Mama una faraja
    Unang'ara sana unavyopendeza
    Moyo wako Mama mpenzi Maria
    Ni msafi kweli unameremeta
  3. Moyo wako mama, umekingiwa
    Dhambi ya asili tuliyoirithi
    Moyo wako mama ni mtakatifu
    Umejaa neema neema teletele
  4. Moyo wako mama, kama waridi
    Unafurahisha unametameta
    Moyo wako mama, kama dhahabu
    Ing'arayo sana mfano wa kioo
  5. Moyo wako mama, ni mtii sana
    Moyo wako mama mtulivu kabisa
    Moyo wako mama ni nuru njema
    Ituongozayo kufika Mbinguni
  6. Moyo wako mama, ni mnyenyekevu
    Moyo wako mama una heri tele
    Moyo wako mama ni wa amani
    Moyo wako mama una neema ya Mungu
  7. Tuombee mama yetu Maria
    Tuombee mama kwa mwanao Yesu
    Ili atakase mioyo yetu
    Ifanane nawe mama yetu mpenzi