Login | Register

Sauti za Kuimba

Tumshangilie Maria Lyrics

TUMSHANGILIE MARIA

 1. Ni Maria mtakatifu, tumshangilie Maria
  Ni mzazi wa Mungu Mwana
  Ni mkuu wa mabikira
  Ni mama yake Yesu Kristu

  Vigelegele vifijo na makofi
  Hoye hoye nderemo nyingi
  Pia vifijo tumshangilie Mama Maria
  Yeye ni mwombezi wetu na msaada
  Njooni tumwimbie chereko mama

 2. Mama wa neema ya Mungu -
  Mama mtakatifu sana -
  Mama wa usafi wa moyo -
  Mama usiye na doa -
 3. Ni mama usiye na dhambi
  Pia mama mpendelevu
  Ni mama msaada wetu
  Ni mama wa shauri jema
 4. Ni Mama wa Muumba wetu
  Pia mama wa Mkombozi
  Bikira wa utaratibu
  Ni bikira mwenye heshima
 5. Ndiye bikira mwenye sifa
  Ndiye bikira mwenye enzi
  Ni bikira mwenye huruma
  Na ndiye bikira amini
 6. Na ndiye kioo cha haki
  Ni kikao chenye heshima
  Sababu ya furaha yetu
  Ndiye chombo chenye rehema
 7. Ndiye chombo chenye heshima
  Ni chombo chema cha ibada
  Ndiye waridi lenye fumbo
  Ndiye manara wa Daudi
 8. Yeye ni mnara wa pembe
  yeye ni nyumba ya dhahabu
  Ndiye sanduku la agano
  Yeye ni mlango wa mbingu
 9. Ndiye nyota ya asubuhi
  Yeye ni afya ya wagonjwa
  Kimbilio la wakosefu
  Mfariji wa wenye uchungu
 10. Ni msaada wa Wakristu
  Malkia wa malaika
  Ndiye malkia wa mababu
  malkia wa manabii
 11. Ndiye malkia wa mitume
  Malkia wa mashahidi
  Malkia wa waungama
  Malkia wa mabikira
 12. Malkia wa watakatifu
  Aliyepalizwa mbinguni
  Ni wa Rosari takatifu
  Ndiye Malkia wa amani
Tumshangilie Maria
ALBUMUwe Nasi Mama Maria
CATEGORYBikira Maria
SOURCEArusha Tanzania
 • Comments