Mama wa Msaada

Mama wa Msaada
Performed by-
AlbumUwe Nasi Mama Maria
CategoryBikira Maria
Views4,415

Mama wa Msaada Lyrics

  1. Mama wa msaada Maria tusaidie
    Maombezi yako Maria ni nguzoyetu
    Tutangulie mama katika safari
    ya kwenda Mbinguni tuongoze mama

  2. Mama mwenye huruma msaada wetu Wakristu
    Mama simama mbele yetu nasi tuwe nyuma yako tunaposafiri
  3. Tunatumaini kwako, kutukumbatia wanao
    Twajua ni wewe mama yetu tunapokulilia mama usituache
  4. Tulitaje jina lako kwa taji wote
    Twajua wewe ndiwe mwombezi wetu tuweze shinda maovu tunaposafiri