Login | Register

Sauti za Kuimba

Kwa Nini Wasimama Mbali Lyrics

KWA NINI WASIMAMA MBALI

@ D. Mlolwa

Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
Ee Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
{ Kwa nini kujificha na kujificha nyakati za shida
Kwa nini kujificha Bwana nyakati za shida } *2

 1. Kwa kiburi chake mtu asiye haki
  Mnyonge anafuatiwa anafuatiwa kwa ukali
  Na wanasema hila hizo hizo walizoziwaza
 2. Maana mdhalimu, mdhalimu hujisifia
  Hujisifia sifia tamaa ya nafsi yake
  Na mwenye uchoyo humkataa Bwana na kumdharau
 3. Asema moyoni mwake, asema sitaondoshwa
  Kizazi hata kizazi, sitakuwapo taabuni
  Kinywa chake kimejaa laana na hila na dhuluma
Kwa Nini Wasimama Mbali
COMPOSERD. Mlolwa
CHOIRSt. Maurus Kurasini
ALBUMHubirini Kwa Kuimba
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
MUSIC KEYA Major
TIME SIGNATURE3
8
SOURCETanzania
NOTES Open PDF
 • Comments