Kwa Nini Wasimama Mbali

Kwa Nini Wasimama Mbali
Performed bySt. Maurus Kurasini
AlbumHubirini Kwa Kuimba
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerD. Mlolwa
VideoWatch on YouTube
Views14,207

Kwa Nini Wasimama Mbali Lyrics

  1. Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
    Ee Bwana ee Bwana, kwa nini wasimama mbali
    { Kwa nini kujificha na kujificha nyakati za shida
    Kwa nini kujificha Bwana nyakati za shida } *2

  2. Kwa kiburi chake mtu asiye haki
    Mnyonge anafuatiwa anafuatiwa kwa ukali
    Na wanaswe kwa hila hizo hizo walizoziwaza
  3. Maana mdhalimu, mdhalimu hujisifia
    Hujisifia sifia tamaa ya nafsi yake
    Na mwenye uchoyo humkataa Bwana na kumdharau
  4. Asema moyoni mwake, asema sitaondoshwa
    Kizazi hata kizazi, sitakuwamo taabuni
    Kinywa chake kimejaa laana na hila na dhuluma