Yesu Kristu Atawala
Yesu Kristu Atawala | |
---|---|
Performed by | Kwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha |
Album | Asante Mungu |
Category | Kristu Mfalme (Christ the King) |
Composer | S. G. Ngagaja |
Views | 4,588 |
Yesu Kristu Atawala Lyrics
Yesu Kristu atawala milele yote
Yesu Kristu ndiye Bwana wa mabwana wote
Yesu Kristu atawala milele yote
Yesu Kristu ni mfalme wa wafalme wote
Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliyetukomboa kwa damu yake
Mataifa njooni tumwimbie
Tumfanyie shangwe Mungu wetu
Tuzitangaze rehema zake, pia na utukufu wake
Ili mataifa yote duniani
Yapate kumjua Bwana
Nao wote waliopotea, waweze kumrudia Mungu- Alikuja duniani, kwa ajili yao,
ili mi niliye mdhambi nipate kuokolewa
Alipata mateso mengi kwa ajili yangu mimi - Tazama uwezo wake, Mwana wa Mungu
Limfufua Lazaro kutoka katikati ya wafu
Tazama na yule kipofu, alimponya akapona - Alifanya miujiza mingi duniani
Alitoa pepo wachafu, aliponya na wagonjwa
Aliyakemea mawimbi, bahari ikawa shwari - Njoo sasa ndugu yangu, kwake Bwana Yesu
Tatizo lako lolote ulilo nalo litakwisha
Njoo ufanyiwe maombi kwa Yesu yote yawezekana