Yesu Kristu Atawala

Yesu Kristu Atawala
ChoirKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
AlbumAsante Mungu
CategoryKristu Mfalme (Christ the King)
ComposerS. G. Ngagaja
SourceArusha Tanzania

Yesu Kristu Atawala Lyrics

Yesu Kristu atawala milele yote
Yesu Kristu ndiye Bwana wa mabwana wote
Yesu Kristu atawala milele yote
Yesu Kristu ni mfalme wa wafalme wote

Yeye ndiye Mwana wa Mungu aliyetukomboa kwa damu yake
Mataifa njooni tumwimbie
Tumfanyie shangwe Mungu wetu
Tuzitangaze rehema zake, pia na utukufu wake
Ili mataifa yote duniani
Yapate kumjua Bwana
Nao wote waliopotea, waweze kumrudia Mungu

 1. Alikuja duniani, kwa ajili yao,
  ili mi niliye mdhambi nipate kuokolewa
  Alipata mateso mengi kwa ajili yangu mimi
 2. Tazama uwezo wake, Mwana wa Mungu
  Limfufua Lazaro kutoka katikati ya wafu
  Tazama na yule kipofu, alimponya akapona
 3. Alifanya miujiza mingi duniani
  Alitoa pepo wachafu, aliponya na wagonjwa
  Aliyakemea mawimbi, bahari ikawa shwari
 4. Njoo sasa ndugu yangu, kwake Bwana Yesu
  Tatizo lako lolote ulilo nalo litakwisha
  Njoo ufanyiwe maombi kwa Yesu yote yawezekana