Aleluya Mimi Ndimi Chakula

Aleluya Mimi Ndimi Chakula
ChoirKwaya ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Unga Limited Arusha
AlbumAsante Mungu
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerAjabu J. Ndahitobhotse
SourceArusha Tanzania

Aleluya Mimi Ndimi Chakula Lyrics

Aleluya aleluya, mimi ndimi chakula
Chakula chenye uzima
Mtu akila chakula, akila chakula hiki
ataishi milele
Aleluya - aleluya, aah, aleluya
Aleluya, aleluya aleluya

 1. Twaeni twaeni aee huu ndio mwili ae
  Mpate uzima wa milele, wa milele
 2. Akatwaa kikombe aee, akashukuru aee
  Akawapa wakinywe wote, wakinywe wote
 3. Tumshangilie aee, tupige makofi aee
  Tukampokee huyu Yesu, mtetezi wetu

  //hitimisho//
  Huyu ndiye Yesu Kristu hoiye, haya haya
  Tumpokee kwa upendo hoiye, haya haya
  Huyu ndiye Yesu Kristu hoiye, haya haya
  Tumpokee kwa upendo hoiye, haya haya
  hoiye Yesu haya haya
  ni shangwe ni shangwe
  Hakika Yesu ndiye Bwana, mwana wa Mungu
  Ndiye anayetufungulia mbingu
  aee ee ee
  Aleluya - aleluya, aah, aleluya
  Aleluya, aleluya aleluya


In the tune of Astahili Mwanakondoo