Nimeingia Mahali Hapa
| Nimeingia Mahali Hapa |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Entrance / Mwanzo |
| Composer | E. I. Kalluh |
| Views | 8,002 |
Nimeingia Mahali Hapa Lyrics
Nimeingia mahali hapa patakatifu,
kuja kumwabudu Bwana
{Amani na iwe ndani ya ngome zako
Na salama ndani ya nyua zako } *2
- Makao yako yapendeza sana,
Ee Bwana Mungu wa majeshi
Nakipenda kikao cha nyumba yako
Na mahali pa hema ya utukufu wako
- Nalifurahi waliponiambia
Tutaingia nyumbani kwa Bwana
Sasa miguu yetu imesimama
Katika milango yako ee Yerusalemu
- Ee Mungu wangu
Muumba wangu
Kuwe furaha yangu
Nikutumikie kwa moyo mkunjufu mimi mwanao