Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio
Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio |
---|
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Victor Aloyce Murishiwa |
Views | 7,576 |
Mchaka Mchaka Twendeni Mbio Mbio Lyrics
- La mgambo sasa limelia tembea ndugu yangu tena ukaze mwendo
Safari yetu bado ni ndefu tushikane tutembee pamoja
Milima pia nayo mabonde, tazama visije kuwa ni vikwazo kwako
Ubebapo Neno lake Mungu songa mbele usirudi nyuma
{Hima hima twendeni kwa pamoja
Mchaka mchaka twendeni mbio mbio
aee iye ye he he he hehe
aee iye ye he he he iye
Twendeni wote mbinguni kwa Baba} *2
- Watu wengi wana mali nyingi lakini kutoa sadaka kwao ni ndoto
Wengi wao bila kuogopa humpa Mungu wao chenji
Wengine huwatesa wajane jamani tena kuwanyanyapaa yatima
Ikiwa unaitamani mbingu tenda wema na twende pamoja
- Tuzingatie tabia yako nao wale wenzetu pia tuwasaidie
Badala ya kusubiri wafe na kutazama kwenye misiba
Kumbukeni maneno ya Yesu aliyonena kupitia Injili Luka
Mimi nilipokuwa mgonjwa hamkuja kunitazama
- Wengine wamekataa toba husema siwezi kutubu kwa mwanadamu
Wamesahau ya kwamba Mungu alituachia makasisi
Amewapatia mamlaka hakika watakalolifunga duniani
Na mbinguni pia itafungwa ole wenu mnaowadharau