Njooni Tushukuru
Njooni Tushukuru Lyrics
- Watu wote njooni tushukuru, njooni tushukuru aee,
Simameni tuseme asante, tuseme asante aee
{Na tuimbe - kwa vigelegele
Na tucheze - ngoma na vinanda
Kwa vinubi, zeze na filimbi aee } *2
- Yeye ndiye aliyeziumba, mbingu na dunia aee
Vitu vyote vionekanavyo, na visivyoonekana
- Kwa mfano wake katuumba, tufanane naye aee
Ametupa vyote tutawale, tumtumikie aee
- Shukuruni Mungu wa miungu, Bwana wa mabwana aee
Zitoeni dhabihu za shangwe, za kumshukuru aee
- Tukuzeni Mungu siku zote, daima milele aee
Msifuni kwa kila sauti hata kwa ukimya aee