Furaha Yako
Furaha Yako | |
---|---|
Performed by | St. Anna Hananasif Kinondoni Dsm |
Album | Tuchome |
Category | Tafakari |
Composer | E. A. Minja |
Views | 4,329 |
Furaha Yako Lyrics
Kuna kitu wewe wawaza
(na pia) kuna kitu wewe wapenda
(Tazama) kuna kitu wewe wataka
daima mchana usiku wawaza
(Na sasa) ukipata unafurahi
(kuliko) nazo shida kuzisahau
(Tazama) moyo hujawa na furaha
na kumbe matatizo unaongeza
Ukienda huku we - barabara ni yako we
Ukirudi huku lo - barabara ni yako tu
Kwenye kuongea we - tunajua ni wewe tu
Na kwenye kelele -tunajua ni wewe tu
Ukienda huku we - mbele kweli yako we
Ukirudi huku lo - katikati chako we
Ukienda kule ee - na ulafi ni wako we
Ukifurahia ee - nayo gongo ni yako eh!
Unachokijua kimoja - ulevi,
nyumba imekuwa ni fujo,
(Tazama) Kelele huzuni na kero,
sababu ya kukarabati mizigo
(Najua) kazi hiyo aliyekupa ni nani,
shetani mpenda tamaa
(Huoni) amani upendo huruma hakuna,
huwezi kupata furaha- [s]
Unapokipata kinywaji, kazi yako wewe ni moja
Wenzako wakipata kiu, wewe unamiminia
Furaha yako iliyoje, kujiburudisha na pombe
[b]
Itazame na afya yangu, na sasa inayo migogoro
Chakula kwangu siyo kitu, pombe na mimi mimi na pombe
Hata na maendeleo yangu yamekuwa ni ya kuzorota - Itazame na nyumba yetu, amani upendo hakuna
Watazame watoto wetu, afya yao inavyoyumba
Nguo zao sasa ni duni, viraka vina mkutano
Nikitazama ndoa yangu, ni lawama na ni lawama
Kurudi kwangu ni usiku, tena usiku wa maneno
Nina shtuma kama shindano, huyu maarufu gani tena? - Uurudishe moyo nyuma, ukabadilike mwenendo
Familia uitazame, ndoa nayo uijali
Watoto msingi wa kesho, maendeleo wajengee
Kumbe kweli nilipotea, na kuyasahau majukumu
Familia hata ndoa yangu, nilitelekeza kwa ulevi
Hata na mlango wa kanisa na jumuiya sikukumbuka