Nakupenda Maria

Nakupenda Maria
ChoirSt. Cecilia Mwenge Dsm
AlbumNakupenda Maria
CategoryBikira Maria
ComposerP. F. Mwarabu

Nakupenda Maria Lyrics

{ Nakupenda Maria Mama uliye bora ,
Furaha yangu Maria nikae nawe daima ,
Nipate neema zako nifike juu mbinguni } *2

  1. Mama mwema Mariaunikinge unilinde ,
    Nifanye yote mema nayo mabaya niyashinde
  2. Uliye barikiwa Maria mpendelevu ,
    Unijaze Baraka ili niwe mnyenyekevu.
  3. Uyatulize Mama mashaka ya moyo wangu
    Neema za mwana wako zifariji roho yangu