Mpenzi wa Yesu
Mpenzi wa Yesu |
---|
Performed by | - |
Album | Bikira Maria |
Category | Watakatifu |
Views | 2,534 |
Mpenzi wa Yesu Lyrics
Mpenzi wa Yesu tusaidie ,
Mama Theresia tusimamie *2
- Ewe Theresia Mtakatifu
Twakujia wewe mwaminifu
Jionyeshe kwetu sisi wanao
Tusaidie kwa neema za Mungu
- Ewe Theresia duniani humu,
Umeishi kwa unyenyekevu
Tufanyayo twayatolea kwako
Yakoleze yawe kama yako
- Uliteseka mateso mengi sana
Kwa ajili ya Yesu mpenzio
Tusaidie kukubali mateso
Tuwe nasi wapenzi wa Yesu
- Ulitumwa kuwafundisha watu
Njia Ndogo kumwendea Yesu
Nasi utufundishe Njia yako
Tuzifuase fadhila zako
- Mama Theresia mataifa yote
Wewe Mlinzi Msimamizi
Fukuza giza lote mioyoni
Tunyeshee yako mawaridi
- Theresia mwema tusaidie ,
Saa ya kufa kwetu ikiwadia ,
Ili nasi tuseme kama wewe ,
Ee mungu wangu ninakupenda