Mshangilieni Bwana Enyi Nchi Yote
Mshangilieni Bwana Enyi Nchi Yote |
---|
Performed by | - |
Category | Zaburi |
Composer | M. B. Syote |
Views | 2,925 |
Mshangilieni Bwana Enyi Nchi Yote Lyrics
- Mshangilieni Bwana enyi nchi zote
Mtumikieni Bwana kwa furaha
Ingieni kwa shangwe mbele ya uso wake
Jueni kwamba ndiye Mungu wetu
- {Yeye ametuumba na sisi tu mali yake
Kabila lake na kondoo wa malisho yake}*2
Ingieni malango yake malango yake kwa shangwe
Sebule zake kwa kuimba
- Mtukuzeni Bwana, lisifuni Jina lake
- Kwa maana Bwana ni mwema huruma yake yadumu milele
Na uaminifu wa Bwana ni kwa kizazi hata kizazi