Bwana Nikufananishe Na Nini
| Bwana Nikufananishe Na Nini | |
|---|---|
| Performed by | St. Cecilia Kijenge | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Composer | Deo Kalolela | 
| Views | 12,201 | 
Bwana Nikufananishe Na Nini Lyrics
- Bwana nikufananishe na nini
 Au nikufananishe na nani
 Pendo lako Bwana ni la ajabu
 Ndiyo sababu ya furaha yangu
- Kwa kuwa Bwana ulinijua
 Tangu tumboni mwa mama yangu
 Ukanitunza kwa upendo
 Ukanijaza pendo lako
- Nilipokuwa kwenye mateso
 Nilifikiri umeniacha
 Mawazo yangu ya kitoto
 Sikutambua pendo lako
- Kwangu ulijifunua Bwana
 Moyo wangu ulikutambua
 Matendo mengi yenye nguvu
 Uliyotenda mbele yangu
 
  
         
                            