Ndio Mkate wa Malaika

Ndio Mkate wa Malaika
Performed bySt. Antony of padua Magomeni
AlbumTwende Mezani
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerJoseph Makoye
Views4,282

Ndio Mkate wa Malaika Lyrics

  1. Ndio mkate wa malaika, chakula cha wasafiri
    Wenye raha ya milele, sio mkate wa kafiri

  2. Alhamisi Yesu Mwokozi, alisema kwa sauti
    Huu ndio mwili wangu, haya maneno magumu
  3. Vile vile Mwokozi wetu, alisema kama mwanzo
    Hii ndiyo damu yangu, tufanye hivyo daima
  4. Vyote ni kwa ajili yetu, ni kwa ajili ya wote
    kwa ondoleo la dhambi, twatubu makosa yetu
  5. Twakuomba Yesu Mwokozi, utupe chakula chetu
    tukiwa na moyo safi, utushibishe milele