Kwa Jinsi Ujionavyo

Kwa Jinsi Ujionavyo
Performed bySt. Cecilia Kijenge
CategoryTafakari
ComposerJ. Urassa
Views2,633

Kwa Jinsi Ujionavyo Lyrics

  1. Kwa jinsi ujionavyo (ndivyo) ndivyo ulivyoumbwa
    Tena kwa mfano wake Yesu Kristu Mwokozi wetu
    Furaha leo tuimbe shangwe
    Tupige ngoma filimbi na vigelegele
    Tufurahi tufurahi na Bwana Yesu

  2. Yeye mwenyewe aliona kwa jinsi hii utapendeza
    Sasa mbona wewe wamsahau Bwana Mungu wako
    Waisahau hata Sabato siku ya kumshukuru Mungu
  3. Tusijiongeze vitu vingine ndugu vya kujipamba
    Njoo kwake Bwana Yesu atakupamba upendeze
    Ili uweze kufika kwake Mungu kwenye uzima milele
  4. Ni Yesu Kristu peke yake aliye na upendo zaidi
    Katuandalia karamu kabla ya mauti yake
    Kaibariki kila tuilapo tupate uzima milele
  5. Ulapo bila kustahili ndugu ungoje hukumu yako
    Alisema mwenye moyo safi ajongee mezani
    Siku ile ya hukumu nitamwita kwenye ufalme Mbinguni