Nimetambua Makusudi Ya Bwana
Nimetambua Makusudi Ya Bwana |
---|
Performed by | - |
Album | Ona Wanadamu wa Leo |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Deo Kalolela |
Views | 3,784 |
Nimetambua Makusudi Ya Bwana Lyrics
- Nimetambua makusudi ya Bwana
Kwa wale wote aliowapenda
Bwana huwafanya wapondeke moyo
Huwashusha mbele ya mataifa
Bwana watambua nakupenda
Tegemeo langu liko kwako
Nia zangu zote ziko kwako
Bwana wajua ninapoketi
Pia wajua ninaposimama
Ninakukabidhi moyo wangu
- Walio wake lazima kuteseka
Katika siku zote za maisha
Wajikane na waache ya dunia
Na wajivike misalaba yao
- Machukizo ni lazima yatokee
lakini ole anayeyaleta
Moyo wa mteule hujaa furaha
Akiteswa kwa ajili ya Yesu
- Nitayapokea kwa saburi kubwa
Mateso na machungu ya dunia
Ili nivikwe taji la utukufu
Nitakapofika mbele ya Yesu