Login | Register

Sauti za Kuimba

Nimetambua Makusudi Ya Bwana Lyrics

NIMETAMBUA MAKUSUDI YA BWANA

@ Deo Kalolela

 1. Nimetambua makusudi ya Bwana
  Kwa wale wote aliowapenda
  Bwana huwafanya wapondeke moyo
  Huwashusha mbele ya mataifa

  Bwana watambua nakupenda
  Tegemeo langu liko kwako
  Nia zangu zote ziko kwako
  Bwana wajua ninapoketi
  Pia wajua ninaposimama
  Ninakukabidhi moyo wangu

 2. Walio wake lazima kuteseka
  Katika siku zote za maisha
  Wajikane na waache ya dunia
  Na wajivike misalaba yao
 3. Machukizo ni lazima yatokee
  lakini ole anayeyaleta
  Moyo wa mteule hujaa furaha
  Akiteswa kwa ajili ya Yesu
 4. Nitayapokea kwa saburi kubwa
  Mateso na machungu ya dunia
  Ili nivikwe taji la utukufu
  Nitakapofika mbele ya Yesu
Nimetambua Makusudi Ya Bwana
COMPOSERDeo Kalolela
ALBUMOna Wanadamu wa Leo
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
SOURCETanzania
 • Comments