Anakuja Masiha

Anakuja Masiha
Choir-
CategoryMajilio (Advent)

Anakuja Masiha Lyrics

Anakuja Masiha, anakuja Masiha
Anakuja Bwana mfalme, kutuokoa

 1. Itengenezeni njia yake,
  yatayarisheni mapito yake, anakuja Masiha.
 2. Mabonde yote na yafukiwe,
  na vilima vyote visambazwe, anakuja Masiha
 3. Mioyo yote na itakaswe,
  watu wote na wawe tayari, anakuja Masiha
 4. Dunia itaona salama,
  watu watakuwa na amani, anakuja Masiha
 5. Watu watauona wokovu,
  wokovu utakao kwa Bwana, anakuja Masiha