Itengenezeni Njia ya Bwana

Itengenezeni Njia ya Bwana
Performed by-
CategoryMajilio (Advent)
Views23,770

Itengenezeni Njia ya Bwana Lyrics

  1. { Itengenezeni njia ya Bwana, Bwana apite (mapito yake)
    Yanyoosheni mapito ya Mungu wetu aingie } *2

  2. Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako,
    Atakayeitengeneza njia yako,
    Sauti ya mtu, aliaye nyikani nyikani inasema *2
  3. Ondoka ee Yerusalemu, usimame juu
    Tazama uione furaha,
    Inayokujia, kutoka kwake Mungu, Mungu wako *2
  4. Yajazeni yale mabonde yote yashusheni milima,
    Panyosheni na pale palipopotoka
    Tayarisheni njia na mapito ya Bwana aingie *2
  5. Na watu wote wenye mwili, wataona wokovu,
    Wataona wokovu wake Mungu wetu,
    Kwa sababu yeye atakayetukujia ni mwokozi *2