Itengenezeni Njia ya Bwana

Itengenezeni Njia ya Bwana
ChoirTBA
CategoryMajilio (Advent)

Itengenezeni Njia ya Bwana Lyrics

{ Itengenezeni njia ya Bwana, Bwana apite (mapito yake)
Yanyoosheni mapito ya Mungu wetu aingie } *2

 1. Tazama namtuma mjumbe wangu, mbele ya uso wako,
  Atakayeitengeneza njia yako,
  Sauti ya mtu, aliaye nyikani nyikani inasema *2
 2. Ondoka ee Yerusalemu, usimame juu
  Tazama uione furaha,
  Inayokujia, kutoka kwake Mungu, Mungu wako *2
 3. Yajazeni yale mabonde yote yashusheni milima,
  Panyosheni na pale palipopotoka
  Tayarisheni njia na mapito ya Bwana aingie *2
 4. Na watu wote wenye mwili, wataona wokovu,
  Wataona wokovu wake Mungu wetu,
  Kwa sababu yeye atakayetukujia ni mwokozi *2