Chakula cha Bwana Tayari

Chakula cha Bwana Tayari
ChoirSt. Antony of padua Magomeni
AlbumTwende Mezani
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerG. Matui

Chakula cha Bwana Tayari Lyrics

Chakula cha Bwana tayari, twende tukale,
Ametualika mwenyewe, twende ndugu twende,
Twende na usiogope tupate uzima wa milele.

 1. Bwana anatuita twende, tukale chakula cha Mbinguni
  Tukale kwa imani ndugu tutapata uzima
 2. Twende tukampokee Bwana, akae moyoni mwetu daima
  Tukampokee kwa imani, tutapata uzima
 3. Atatulisha na kutunywesha daima, tutapokea mema ya mbinguni
  Tukale kwa imani ndugu tutapata uzima
 4. Yeye ni shina la uzima mpya, pia ni njia wazi ya mbingu
  Tukale kwa imani ndugu tutapata uzima