Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari
Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari |
---|
Performed by | - |
Category | Ekaristia (Eucharist) |
Composer | F. A. Nyundo |
Views | 5,057 |
Chakula cha Bwana Sasa Kiko Tayari Lyrics
- Chakula cha Bwana, sasa kiko tayari ndugu
Karibuni karibuni twende kumpokea
Nacho kimeshuka kimetoka Mbinguni ndugu
Karibuni karibuni twende kumpokea
Bwana Yesu anatuita twende
Tukale mwili wake
Tukanywe damu yake
Sote twende tukampokee
- Tumekaribishwa kumpokea Mwana kondoo
Karibuni karibuni twende kumpokea
Anayeondoa dhambi zote za ulimwengu
Karibuni karibuni twende kumpokea
- Bwana ndiye njia, ya Mbinguni tukampokee
Karibuni karibuni twende kumpokea
Atuita kwake kula mwili na damu yake
Karibuni karibuni twende kumpokea