Naja Kwako Bwana

Naja Kwako Bwana
Performed by-
CategoryInjili na Miito (Gospel)
Views8,738

Naja Kwako Bwana Lyrics

  1. Naja kwako Bwana, unipokee mtumishi wako *2
    Kuijongea altare yako, ee Bwana unipokee
    Kukutolea sadaka ya misa, ee Bwana unipokee
    Kati ya milango yako, Bwana napita.
    Niwekee mkono wako, nibariki *2

  2. Ninakuja kwako kukusujudia,
    Kukutolea shukrani, sala na maombi yangu *2
  3. Nitakusujudu ee mungu wangu,
    Nifanye toba ya kweli, katika hii nyumba takatifu *2
  4. Nitakuimbia kwa nyimbo nzuri
    Kwa nyimbo nzuri za shangwe,
    Kukuabudu ee Bwana Mungu *2