Nyumbani Mwake Bwana
   
    
     
         
          
            Nyumbani Mwake Bwana Lyrics
 
             
            
- Nyumbani mwake Bwana tuingie kwa furaha.
 Twendeni tumwabudu tunjongee mbele zake. *2
- Njoni tumsujudu yeye aliyetuumba
 Yeye anatawala kwa haki na uamini.
- Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu
 Yeye ni Mungu mwenye radhi nyingi na rehema.
- Bwana ni mtawala amejaa utukufu na mashuhuda
 Yake yastahili imani.
- Yeye ni Mungu wetu wa amani na mapendo
 Yeye ni Mungu mwenye utukufu wa ajabu.
- Tumpigie shangwe mwamba wa wokovu wetu
 Ni Mungu wa ujuzi na ni Mungu wa fahamu.
- Na kwa nyimbo za sifa tujongee uso wake
 Vifijo na nderemo tumsifu Mungu wetu
- Na enyi waadili tukuzeni jina lake
 Mfanyieni shangwe yeye aliyetuumba.