Leo Hii Kuna Mambo
| Leo Hii Kuna Mambo | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Harusi | 
| Views | 3,797 | 
Leo Hii Kuna Mambo Lyrics
- Leo hii kuna mambo, msema kesho ni muongo
 Furaha ya leo ni hakika, furaha shangilieni.
- Nasikia leo kuna shangwe,
 Ni shangwe ya nini jamani, leo hii.
- Mbona nyote mwashangilia
 Furaha yote ni ya nini, leo hii
- Kumbe leo kuna harusi
 Ndiyo maana mwashangalia, leo hii
- Hakika na tufanye shangwe
 Tuwapongezeni wenzetu, leo hii
- Nanyi Bwana na Bibi harusi
 Furahi na kushangilia,leo hii
 
  
         
                            