Login | Register

Sauti za Kuimba

Wawili Wakitembea Pamoja Lyrics

WAWILI WAKITEMBEA PAMOJA

Ukiona wawili wakitembea pamoja,
hao kweli wameamua waishi pamoja.
Kweli hawezi tembea pamoja,l
hawajakubaliana;
kweli (hawa, wamekubaliana waishi pamoja kwa upendo *2)

 1. Tunamuona huyu ndugu, wameshikana na huyu dada;
  wakitembea pamoja, (unyo unyo unyo unyo),
  hawa kweli Bwana na Bi Arusi.
 2. Mungu Baba awajalie, maisha mema katika ndoa;
  wapendane siku zote, (pendo pendo pendo pendo),
  vile wewe wpenda kanisa.
 3. Ndugu mpende mke wako, vile Yesu apenda kanisa;
  nawe dada mtii, (mume mume mume wako) mjenge familia pamoja.
 4. Wape watoto Ee Mungu, kama pendo lako kwao;
  nao waimbe nyimbo nzuri,(ti ri ri ri ri ri ri ri ri),
  wakusifu milele yote.
Wawili Wakitembea Pamoja
CATEGORYHarusi
 • Comments